Tanzania yafungua ubalozi wake Israel, Mahiga aomba Israel ifungue ubalozi Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga amezindua rasmi ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Israel na kuitaka Israel nayo iharakishe kufungua ofisi ya ubalozi nchini Tanzania.
Afisi hizo za kibalozi zinapatikana katika mji wa Tel Aviv.
Rais Magufuli mwezi Machi mwaka huu alikuwa amemualika Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutembelea Tanzania na pia kuanzisha ofisi ya ubalozi nchini Tanzania badala ya kutumia ofisi za ubalozi zilizopo Nairobi nchini Kenya.
Waziri Mahiga, akizindua ubalozi huo Jumanne, alisema Watanzania hawataisahau Israel kwa kuwa ndiyo nchi iliyoisaidia Tanzania kuanzisha Jeshi la Kujenga Taifa ambalo mafanikio na mchango wa jeshi hilo unajulikana na kila Mtanzania.
Alisema JKT baada ya lugha ya Kiswahili ndiyo chombo cha pili kilichosaidia kwa kiasi kikubwa kuunganisha makabila zaidi ya 120 ya Watanzania na kuwa wamoja hadi leo.
Sherehe za ufunguzi wa ubalozi huo zilihudhuriwa na Waziri wa Sheria wa Israel Ayelet Shaked.
Dkt Mahiga alisema Israel ni nchi ya kupigiwa mfano kwa sababu licha ya changamoto za kimahusiano na baadhi ya jirani zake bado nchi hiyo imepiiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo cha umwagiliaji.
Aidha, imepiga hatua katika sekta ya viwanda, matibabu, teknolojia ya habari na mawasiliano, ulinzi na usalama, uhifadhi wa maji na masuala ya nishati ikiwemo nishati ya kutumia joto ardhi.
Ufunguzi wa ubalozi huo ni muendelezo wa juhudi za kuimarisha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili ambazo zilitiwa nguvu na ziara ya mawaziri wawili wa Israel nchini Tanzania mwezi Machi.
Waziri wa Ulinzi Avigdor Liberman alizuru Tanzania tarehe 20 hadi 22 Machi 2018 naye mwenzake wa Sheria Ayelet Shaked akafanya ziara ya kukazi tarehe 23 na 24 Aprili 2018.
Katika mkutano na Bw Lieberman ikulu ya Dar es Salaam, Rais Magufuli alikuwa ametaka makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Israel katika maeneo mbalimbali yakiwemo ulinzi na usalama, mafunzo na masuala ya kiuchumi yatiwe saini haraka ili utekelezaji uanze mara moja.
"Tanzania na Israel ni marafiki wa miaka mingi, nataka kuona urafiki wetu unakuwa zaidi, nawakaribisha wawekezaji kutoka Israel kuja kuwekeza katika kilimo, madini na gesi na pia kuwepo ndege za moja kwa moja kutoka Israel hadi Dar es Salaam na Kilimanjaro ili kukuza utalii" alisema Dkt Magufuli.
Katika ziara hizo masuala mbalimbali yaliafikiwa ikwemo Israel kuisaidia Tanzania kuanzisha chombo cha kutoa msaada wa kisheria kwa wasiojiweza ambacho kwa upande wa Israel kimeshaanzishwa na kina mafanikio makubwa.
Dkt Mahiga na Waziri wa Sheria wa Israel Bi Ayelet ShakedHaki miliki ya pichaFOREIGN TANZANIA
Image captionDkt Mahiga na Waziri wa Sheria wa Israel Bi Ayelet Shaked
Dkt Mahiga, akuzungumza Jumanne aliwakaribisha Waisrael kuja Tanzania kwa ajili ya kufanya utalii kwa kuwa Tanzania ina vivutio lukuki vya utalii.
Alisema zaidi ya watalii 50,000 hufika Tanzania kila mwaka lakini hawatoshi kutokana na wingi wa vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: