Mojawapo ya jamii wa awali wa dinosaria alikuwa na maumbile yanayofananishwa na mamba, matokeo ya utafiti Tanzania yanaonyesha.
Wataalam wa masuala ya uhifadhi wa mabaki ya wanyama wamejiuliza familia ya dinosari wa kitambo walifanana vipi, kwani maelezo ya rekodi kutoka enzi hizo ni nadra.
Wengine walidhania walitembea kwa miguu miwili, wakifanana kama dinosari wadogo.
Lakini mnyama mpya aliyeelezewa alitembea kwa miguu minne kama mamba, nakala ya Nature iliripoti
Mnyama huyo mla nyama mwenye urefu wa kati ya mita 2-3 aliyevumbuliwa Tanzania kusini, aliishi takriban miaka milioni 245 iliyopita wakati wa kipindi cha kwanza cha maisha yao (Triassic)
0 Post a Comment:
Post a Comment