“Nchi hii inavunja katiba tuseme kweli siku moja hiki chuo kitengeneze kongamano la kujadili kesi stadi za kuvunja Katiba, siyo kuambaa ambaa tu na kufanya majadiliano haya ya jumla ambayo hayaendani na chuo hiki,” amesema Butiku.
Mchakato wa Katiba Mpya ulifikia hatua ya kupatikana kwa rasimu ya mwisho ya katiba hiyo uliokamilika 2014.
Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete alikabidhiwa rasimu hiyo huku tume hiyo ikitakiwa kuendelea kubaki. Lakini alipochaguliwa Rais wa awamu ya tano, John Magufuli alisema kwa sasa anaangalia zaidi namna ya kuijenga nchi kuliko katiba hiyo.
0 Post a Comment:
Post a Comment