MWANAUME AATAMIA MAYAI YA KUKU UFARANSA


Abraham Poincheval Paris, Ufaransa Machi 29, 2017.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionAbraham Poincheval akiwa anatamia mayai katika makumbusho ya Paris

Msanii kutoka Ufaransa Abraham Poincheval anaendelea kutamia mayai ya kuku akiwa na matumaini kwamba mwishowe yataangua vifaranga.
Msanii huyo anatumia joto kutoka kwa mwili wake kutamia mayao hayo 10.
Poincheval ambaye hufanya uigizaji wa kuigiza mambo ya ucheshi lakini ya hatari tayari ameishi wiki mbili ndani ya dubu, miongoni mwa mambo mengine ya kushangaza.
Atakuwa katika chumba maalum ambacho anatamia mayai, ambapo watalii wanaweza kumtazama katka makumbusho ya Palais de Tokyo mjini Paris.
Anatarajia kutamia mayai hayo kwa siku 21 hadi 26.
"Kusema mweli, kimsingi, ni kama nimekuwa kuku," anasema.
Poincheval, 44, ameuita uigizaji huo wake - "Oeuf" (Yai kwa Kifaransa).
Badala ya kutamia mayai hayo kwa kuchutuma juu yake moja kwa moja, anatumia kiti maalum ambacho kina mfuko eneo lake la kukalia. Hapo ndipo mayai hayo yamewekwa.
Poincheval atakuwa amejifunga blanketi kuzuia joto kupotea.
Aidha, anapanga kula vyakula vinavyoongeza sana joto mwiliki, kama vile tangawizi.
Wakati wa haja, atatumia kijisanduku kidogo kilichomo mvunguni mwa kiti chake.
Ndipo mayai hayo yaangue vifaranga, hahitaji kuondoka zaidi ya dakika 30 kwa siku. Anapanga kutumia muda huo kula chakula.
Uigizaji wa sasa wa Poincheval anaufanya baada ya uigizaji wake aliouita "Pierre" (Jiwe kwa Kifaransa), ambapo aliishi ndani ya jiwe kubwa lililokuwa limechongwa sehemu ya kutoshea mwili wake ndani.

Abraham PoinchevalHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMsanii huyo alikaa ndani ya jiwe kwa wiki moja
Abraham PoinchevalHaki miliki ya pichaAFP
Image captionPoincheval pia alikaa wiki moja juu ya boriti ya urefu wa mita 20 nje ya kituo cha treni cha Gard du Nord mjini Paris
Abraham PoinchevalHaki miliki ya pichaAFP
Image caption...alikaa pia siku 13 ndani ya dubu
Abraham PoinchevalHaki miliki ya pichaAFP
Image caption...alisafiri pia kwenye mto Rhone akitumia chpa kubwa ya plastiki iliyokuwa imefungwa kwa kifuniko
Abraham PoinchevalHaki miliki ya pichaAFP
Image caption... na aliishi ndani ya shimo wiki moja kwenye duka moja la vitabu Marseilles. Wakati mmoja, alitembea kutoka upande mmoja wa Ufaransa hadi mwingine bila kujipinda, akitumia dira kumuongoza.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: