TRUMP: Tutaidhibiti Korea kaskazini



Marekani inaona kuwa kwa muda mrefu Diplomasia ya magharibi imeshindwa kuidhibiti Korea kaskaziniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMarekani inaona kuwa kwa muda mrefu Diplomasia ya magharibi imeshindwa kuidhibiti Korea kaskazini
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Marekani itajiandaa yenyewe kuchukua hatua dhidi ya vitisho vya Nuklia vinavyoonyeshwa na Korea kaskazini.
Katika mahojiano na Gazeti la Financial Times, Trump amenukuliwa akisema ''kama China haitafanya chochote dhidi ya Korea kaskazini, sisi tutafanya''.
Majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliyotekelezwa na Korea kaskazini, yatawaleta ana kwa ana kwa mara ya kwanza Trump na mwenzake wa China Xi Jinping.
kabla ya mkutano wa juma hili mjini Florida, washauri wa masuala ya usalama nchini Marekani wameelezwa kuharakisha kukamilisha orodha ya sera zilizopendekezwa.
Katika ziara yake ya kwanza katika bara la Asia, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson amesema diplomasia ya miaka 20 ya nchi za magharibi iliyolenga kuidhibiti Korea kaskazini imeshindwa.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: