Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis anataka mjadala wa kimataifa uandaliwe wa kususluhisha mvutano unaozidi kutokota kati ya Marekani na Korea kaskazini akisema kwamba swala hilo limekuwa kaa la moto.
Papa Francis amewaambia wanahabari kwamba mzozo baina ya mataifa hayo huenda ukazua vita vitakavyoangamiza watu wengi.
Amesema kwamba umoja wa mataifa umepoteza nguvu zake.
Awali manowari ya kivita ya Marekani iliwasili karibu na rasi ya Korea, saa chache baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la kombora ambalo lilitibuka.
Rais wa Marekani Donald Trump ameishutumua Korea Kaskazini kwa kuiokosea heshima jirani wake China na rais wake.
Hivi majuzi Trump alimulika rais wa China Xi Jinping na kumpongeza kwa kujitahidi kutatua mzozo wa Korea Kaskazini.
Jaribo la kombora la Korea Kaskazini lilijiri saa chache baada ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa kujadili mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini
0 Post a Comment:
Post a Comment