Utafiti: Simu aina ya smartphone kudhibiti kisukari

  • 29 Aprili 2017


Simu aina ya smartphone
Simu aina ya smartphone

Simu moja aina ya smartphone(maarufu kama simu za kupangusapangusa) imechukuwa jukumu muhimu katika majaribio ambayo huenda yakawasaidia mamilioni ya watu duniani ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa kisukari kuweza kudhibti kiwango cha sukari.
Watafiti wa China katika jarida la sayansi wanasema walivumbua seli za insulini na kuzidunga ndani ya panya ili kufanya kazi wakati zinapoangazwa na mwanga wa LED.
Mwanga huo ulizalishwa na programu ya simu hiyo aina ya smartphone baada ya kupokea data kutoka kwa kifaa cha kupimia damu ilio na sukari ndani ya panya huyo.
Kwa sasa watu walio na kisukari hupimwa damu ili kubaini ni wakati gani wanahitaji sindano za insulini.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: