Ngumi kurindima Dar





. Mashindano ya taifa ya ngumi yanatarajiwa kuanza leo kwenye viwanja vya Tanganyika Packers jijini huku mabondia kutoka vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama wakitarajiwa kutamba.
Katibu mkuu wa shirikisho la ngumi Tanzania (BFT), Makore Mashaga alisema mashindano hayo yatafunguliwa saa nane mchana kwenye viwanja hivyo, baada ya zoezi upimaji uzito kukamilika.
"Mabondia wataanza kupima uzito palepale Tanganyika Packers asubuhi saa tatu na baada ya hapo ratiba ya mashindano itatolewa rasmi tayari kwa mabondia  kuingia ulingoni mchana," alisema Mashaga.
Rais wa BFT, Mutta Lwakatare alisema kuwa mashindano hayo ndio yatakayotumika kupata timu ya taifa ya ngumi itakayoshiriki mashindano ya Afrika.
"Safari hii tunataka kutengeneza timu ya taifa ambayo itakwenda kufanya vizuri na ndio maana mashindano haya tumeyafanya mapema ili tupata muda wa kutosha wa maandalizi.
"Nina imani kuwa katika mashindano ambayo tutakwenda kuwakilisha taifa letu, safari hii tutafanya vizuri kwa kuwa tumepata wawakilishi wazuri," alisema Lwakatare.



                                                         Comment, like and share
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: