Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani amesema ujenzi wa nyumba za viongozi katika maeneo mapya ya utawala kwenye mikoa 20 umesimama kutokana na ukosefu wa fedha.
Ngonyani amesema hayo jana alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbogwe (CCM), Augustino Masele aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuanza ujenzi wa nyumba ya makazi ya mkuu wa Wilaya Mbogwe ambayo inajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Ngonyaji amesema katika mwaka wa fedha wa 2013/14, Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ilitenga fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa nyumba 149 za viongozi kwenye mikoa hiyo.
Amesema mradi huo ulihusisha ujenzi wa nyumba nne za wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya 21, makatibu tawala wa mikoa wanne, makatibu tawala wasaidizi wa mikoa 40, makatibu tawala wa wilaya 38 na maofisa waandamizi 42.
0 Post a Comment:
Post a Comment