Spika wa bunge katika jimbo la Kano lililoko kaskazini mwa Nigeria, amesema kuwa umma utaombwa kutoa maoni yao kuhusu muswada wenye lengo la kuwazuia wanaume maskini kuoa zaidi ya mke mmoja.Alhassan Rurum aliiambia BBC kuwa viongozi na wasomi wataombwa ushauri kuhusu ni nani haswa atatambuliwa kuwa maskini.
Pendekezo hilo lenye utata lilitolewa na Muhammad Sanusi II, ambaye ni Emir wa Kano, kuhakisha kuwa wanaume wana familia ambazo wanaweza kuzitunza.Tangu aingie madarakani mwaka 2014, Emir Muhammad Sanusi II, amekuwa akitoa mapendekezo mengi yenye utata ambapo amepinga misimamo mingi ya kitamaduni.
0 Post a Comment:
Post a Comment