Akizungumza katika Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Meru, Gambo amesema bandari hiyo itajengwa ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo hususan malighafi za viwanda na bidhaa jambo ambalo litachochea uchumi wa mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
Gambo amesema zaidi ya ekari 500 zitatengwa kwa ajili ya kusaidia kufanikisha mchakato huo.
“Jamani kujengwa kwa bandari hiyo kutasaidia sana kurahisisha maendeleo katika wilaya hii na mkoa wetu ,hivyo tunaomba wananchi wa Arusha mtoe ushirikiano katika kufanikisha suala hili,”
0 Post a Comment:
Post a Comment