Shambulizi la kompyuta kuathiri watu zaidi Jumatatu


14 Mei 2017


Udukuzi wa komputa kuathiri watu zaidi Jumatatu
Haki miliki ya picha
Wataalmu wa usalama katika mitandao ya kompyuta, wanaonya kwamba kunaweza kutokea mashambulio mengine sehemu mbalimbali za dunia, pale watu wataporudi makazini hapo kesho.
Inakisiwa kuwa kompyuta zaidi ya 120 katika nchi kama 100, zilidukuliwa Ijumaa.
Lakini polisi wa Umoja wa Ulaya wanasema walioathirika ni 200,000 katika nchi 150.
Shambulio hilo limeathiri watumizi pamoja na ofisi za serikali, kampuni zinazotengeneza magari, mabenki na huduma za afya.
Shambulio hilo limezuwia kompyuta kufikia data, na wanadai kikombozi, ili kuacha kuikorofisha kompyuta.
Uchambuzi uliofanywa na BBC katika akaunti tatu za sarafu ya kidijitali, bitcoin, unaonyesha washambuliaji wamelipwa kikombozi zaidi ya mara 100, jumla ya dola karibu 30,000.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: