Brigitte! Mke wa kipekee wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron


12 Mei 2017
Brigitte na mkewe MacronHaki miliki ya picha
"Brigitte! Brigitte! Brigitte!" umati uliimba alipopanda jukwaani na mumewe, rais mpya wa Ufaransa Emmanuel Macron. Lakini yeye ni nani?
Jina lake halisi ni Brigitte Trogneux.
Mwanzo kabisa, uhusiano wao si wa kawaida.
Haya ni maneno ya Bw Macron mwenyewe aliyesema kwamba uhusiano wao si wa kawaida siku yao ya harusi.
Kuna pengo la umri la miaka 24 kati ya wawili hao.
Macron ana miaka 39 naye mkewe ana miaka 64.
Tofauti yao katika umri ni sawa na Donald na Melania Trump. Trump ana miaka 70 naye mkewe Melania ana umri wa miaka 47.
Macron alikutana na mkewe alipokuwa mwalimu wake wa uigizaji.
Alikuwa na umri wa miaka 15 na alikuwa mwanafunzi mwerevu sana.
Alikuwa mwanafunzi katika shule ya kibinafsi ya Wajesuiti, Amiens ambapo, Brigitte baadaye alisema "alikuwa na uhusiano wa ngazi sawa alipokuwa anahusiana na watu wazima" badala ya kujichukulia na kuzungumza kama kijana aliyekuwa ndio tu amebalehe.
Alieongeza: "Nilitekwa na werevu wa mvulana huyu."
Jina lake la kuzaliwa ni Brigitte Trogneux, na alikuwa mrithi wa kampuni ya kutengeneza chokoleti ambayo ilikuwa maarufu sana kwa sababu ya macaroon.
Alisoma na kuwa mwalimu wa somo la kuigiza na kisha akaolewa na mfanyakazi wa benki André Auzière.
Walijaliwa watoto watatu.
Wazazi wa Emmanuel waligundua kwamba mtoto wao alikuwa ameingia kwenye mapenzi, lakini yamkini hawakufahamu nani alikuwa mpenzi wake.
Brigitte Macron akiwa Le Touquet 7 MeiHaki miliki ya pich
Image captionBrigitte Macron ana watoto watatu kutoka kwa mume wake wa kwanza
Badala yake, mwandishi wa hadithi kuhusu maisha yake Anne Fulda ameandika, walidhani alikuwa amempenda Laurence Auzière, msichana waliyekuwa katika darasa moja. Lakini, kumbe alikuwa amempenda mamake msichana huyo.
Wazazi wa Macron walipogundua hilo, walimwamuru Brigitte kukaa mbali an mtoto wao hadi afikishe umri wa miaka 18.
"Siwezi kuwaahidi jambo lolote," aliwajibu.
Alipotimiza miaka 17, Emmanuel alikuwa tayari amemwambia Brigitte kwamba angemuoa siku moja.
Ilikuwa ni mwongo mmoja baadaye, mwaka 2007, alipotimiza ahadi hiyo.
Sasa, mamake Macron anasema huwa anamtazama Brigitte "zaidi kama rafiki" badala ya mkazamwana.
Laurence AuzièreHaki miliki ya pic
Image captionLaurence Auzière alikuwa katika darasa moja na Macron. Sasa, Macron ni babake wa kambo
Laurence sasa ameibuka kuwa mmoja wa wanaomuunga mkono zaidi babake wa kambo na alikuwa kwenye mkutano wake wa hadhara Paris kwa mfano.
Mtoto mwingine wa kambo Tiphaine, 32, ni wakili ambaye alifanya kazi katika kundi lake la kampeni.
Wanafamilia wote walikuwa jukwaani Macron alipokuwa anasherehekea ushindi wa urais Jumapili katika eneo la Louvre, Paris.
Rais huyo mteule ana watoto watatu wa kambo na kupitia kwao, wajukuu saba.
Bi Macron alijiuzulu kazi yake ya ualimu baada ya mumewe kuteuliwa kuwa waziri wa uchumi, na akawa mmoja wa washauri wake wakuu.
Macron na TrogneuxHaki miliki ya picha
Image captionMacron atakuwa na mkewe ikulu ya Élysée Palace, na Macron anasema atakuwa na majukumu
Brigitte anasifiwa kwa kuathiri mtazamo wa Macron kuhusu wanawake katika siasa.
Ameahidi kwamba nusu ya watu wote watakaowania nyadhifa chini ya chama chake cha En Marche (Tunasonga) katika uchaguzi wa ubunge mwezi Juni watakuwa wanawake.
Na amesema anataka kufanya rasmi wadhifa na majukumu ya mke wa rais.
Katika mahojiano na Vanity Fair mwezi jana, alisema: "Nikichaguliwa - samahani, tukichaguliwa - atakuwa (Brigitte) hapo, atakuwa na majukumu na nafasi."
Kama mwalimu wa zamani, huenda akaangazia zaidi kuwasaidia vijana akiwa mke wa rais.
Lakini kwa hilo, watu watasubiri.
Bw Macron amependekeza kwamba wadhifa wa mke wa rais hautakuwa na mshahara na kwamba sifa zake zitaongozwa na Brigitte.
"Atakuwepo, na atakuwa na usemi, na mtazamo kuhusu mambo. Atakuwa nami, kama alivyokuwa muda huu wote, atakuwa pia na majukumu mbele ya umma."
Baadhi ya vibonzo Ufaransa vimekuwa vikimtania, na kumuonyesha Macron kama mwanafunzi anayepokea maagizo kutoka kwake.Na mpinzani wake Marine Le Pen wakati mmoja alimshambulia kuhusiana na asili ya uhusiano wao.
Alisema: "Bw Macron … naona unajaribu kuigiza kama mwalimu nami mwanafunzi. Lakini kwangu, siwezi kukubalia hilo."
Bi Macron mwenyewe amedhihirisha kwamba anaweza kucheka suala la umri wao.
Amenukuliwa katika kitabu kimoja akisema: "Anahitaji kuwania urais mwaka 2017 kwa sababu 2022, tatizo lake kubwa litakuwa sura yangu."
Wawili haoHaki miliki ya picha
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: