Mkurupuko mbaya zaidi wa Ebola ulitokea 2014-2015 Afrika Magharibi
Idadi ya watu ambao wamashukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepanda na kufikia 29.
Idadi hiyo imepanda kutoka 21 kwa mujibu wa msemaji wa Shirika la Afya Duniani Christian Lindmeier ambaye amenukuliwa na shirika la habari la Reuters.
Watu watatu wamefariki kutokana na ugonjwa huo kufikia sasa, na wengine 416 ambao walijumuika na waliokuwa wameambukizwa wanatafutwa kuchunguzwa iwapo wana dalili za ugonjwa huo.
Watu walianza kuugua tarehe 22 Aprili katika mkoa wa Bas-Uele kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Eneo hilo lililoathirika linapatikana kilomita 1,300 (maili 800) kaskazini mashariki mwa Kinshasa karibu na mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Afrika ya Kati, eneo lenye misitu.
0 Post a Comment:
Post a Comment