Mwili wa mwanasiasa wa Kenya 'wapatikana mtoni'


20 Mei 2017

Thomas minito
Polisi wanasema wanashuku Thomas Minito aliuawa kutokana na majeraha kichwani.
Polisi nchini Kenya wanasema mwanasiasa aliyehusishwa na uvamizi wa mashamba ya kibinafsi amepatikana ameuawa.
Wanaamini mwili uliotolewa mtoni jana ni wa Thomas Minito, ambaye alikuwa akichunguzwa kwa kujihusisha na kupigwa risasi kwa mhifadhi Mwitaliano Kuki Gallman.
Mwili huo ulipatikana ukielea kwenye mto mmoja eneo la Machakos, kilomita hamsini mashariki mwa Nairobi.
Polisi walisema walimtambua kupitia stakabadhi zilizokuwa mfukoni mwake. Familia yake hata hivyo haijadhibitisha haya.
Polisi wanasema wanashuku aliuawa kwa kuwa alikuwa na majeraha kichwani.
Minito alikamatwa tarehe 30 mwezi Machi na kushtakiwa kwa kosa la kuchochea ghasia katika kaunti ya Laikipia, yaliyofanya mhifadhi mashuhuru wa mazingira na mwandishi, Kuki Gallmann kupigwa risasi.
Polisi wangali wanafanya operesheni katika Kaunti ya Laikipia iliyoko Kenya ya Kati. Hii ni baada ya wafugaji kuvamia mashamba ya kibinafsi wakitafuta lishe. Mmiliki mmoja wa mashamba hayo makubwa aliuawa mapema mwezi Machi, Wafugaji wanadai polisi wamewauwa mamia ya wanyama ili kuwafurusha.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: