Mwanamme amuua mkewe kwa kumpiga risasi kisha naye kujiua


26 Mei 2017


Mkazi wa Mahina, jijini Mwanza, aliyefahamika kwa jina moja la Max, anadaiwa kumuua mke wake, Teddy Malulu kwa kumpiga risasi  usiku wa kuamkia leo.
Baada ya kufanya mauaji hayo, Max naye anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi.
Mpaka sasa chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa  mwanamke anayedaiwa kuuawa na mume wake ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi Tanzania (Tafu) .
Kamanda Msangi amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea. 
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: