14 Mei 2017
Rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ameapishwa juma moja baada ya kupata ushindi mkubwa katika marudio ya uchaguzi mkuu wa Urais nchini humo.
Alimshinda pakubwa kiongozi wa chama cha kulia Bi Marine Le Pen.
Macron na Mkewe
Bwana Macron, ambaye aliendesha siasa zake akiunga mkono umoja wa Jumuia ya mataifa ya Bara Ulaya, ameahidi kufufua uchumi wa Ufaransa na kufanyia mabadiliko siasa za kale za Ufaransa.
Ili kuafikia mabadiliko zaidi, chama chake kipya cha The Republic on the Move, kinafaa kushinda viti vingi vya ubunge katika uchaguzi wa mwezi ujao.
Macron(kushoto) na Hollande
Iwapo Bwana Macron, atashindwa katika wadhifa huu wake mpya kama Rais wa Ufaransa, atakuwa tu sawa na mtangulizi wake wa chama cha Kisosiolosti Francois Hollande, ambaye aliahidi mabadiliko, lakini anaondoka kama Rais asiye na umaarufu katika hostoria ya Ufaransa.
0 Post a Comment:
Post a Comment