Gwajima: Nlikuwa siufahamu mgogoro wa CUF

11 Mei 2017

Maalim Seif akizungumza na Askofu Gwajima 


Askofu Gwajima ameyahoji hayo baada ya kupokea malalamiko ya mgogoro uliopo ndani ya CUF kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad alipokwenda kumtembelea ofisini kwake, leo Ubungo jijini Dar es Salaam.

“Katika mazungumzo yetu nilitaka kujua Lipumba anafanyaje kuvuruga chama chako ili nami nijue cha kufanya, si unajua tena. Kwa nini unamruhusu kukivuruga chama?” amehoji Gwajima.

Baada ya kuhoji hayo, Gwajima amesema atayatafakari mazungumzo hayo na kwamba baada ya kutafakari atajua cha kufanya sambamba na kuueleza umma kile atakacho kuwa nacho.

“Kwa vile ameniambia mgogoro jinsi ulivyo basi nami najua cha kufanya, na nitakacho kuwa nacho nitasema baadae, ngoja nitafakari kwanza,” amesema.

'Mimi huyu ni rafiki yangu kwa hiyo nilitaka kujua Professa Lipumba anafanya nini kuvuruga CUF, hivyo nilitaka kujua Lipumba amepatwa na nini mpaka amevuruga chama chako na kiukweli mimi nilikuwa siufahamu vizuri huu mgogoro ila saizi Seif ameniambia kwa hiyo na mimi nataka nitafakari alichoniambia rafiki yangu ni 'digest' baada ya hapo nitajua nafanya nini" alisema Gwajima

Nilikuwa siufahamu vizuri mgogoro wa CUF ila sasa Seif ameniambia. Natafakari alichoniambia ni 'digest' halafu nitajua nafanya nini - Gwajima

Kwa upande wake Maalim Seif ambaye alizuru kwa Gwajima kwa ajili ya kumjulia hali na kuzungumza naye masuala mbalimbali ya nchi, amesema anamuunga mkono mchungaji huyo kwa chochote atakacho kufanya.

“Namuunga mkono aliyoyasema, sisi ni marafiki wa muda mrefu nimekuja kumjulia hali na kuzungumza naye mambo mbalimbali na kila mmoja kayaeleza yake,” amesema Maalim Seif.

Mshirikishe Mwenzako: zakacheka.blogspot.com

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: