Wanawake Chadema wawabwaga Wenje na Masha ubunge wa Eala


11 Mei 2017

 Wabunge wamewachagua Josephine Lemoyan na Pamela Massay kuwa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala) kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Washindi hao walichuana na Profesa Abdallah Safari, Salum Mwalimu, Ezekia Wenje na Lawrence Masha.
Masha na Wenje, walishiriki uchaguzi uliofanyika Aprili 4 ambao Chadema ilipeleka majina yao pekee jambo lililozua mjadala bungeni na kuhitimishwa kwa wao kupigiwa kura za Hapana.
Katika uchaguzi huo wa awali, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waliwachagua wajumbe saba wa Eala.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah alisema ljana (Jumatano) kuwa, kwa matokeo hayo, wabunge tisa wa Eala kutoka Tanzania ni Lemoyan, Massay, Fancy Nkuhi, Happiness Legiko, Maryam Ussi Yahya, Dk Abdullah Makame, Dk Ngwaru Maghembe, Adam Kimbisa na Mohamed Habib Mnyaa.



Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: