Gwajima, Maalim Seif wazungumzia mgogoro wa CUF


11 Mei 2017




 Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema hakuwa anafahamu kuhusu mgogoro unaoendelea katika Chama cha Wananchi (CUF).
Gwajima baada ya kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kanisani hapo Ubungo jijini hapa amesema  hakuwa akiufahamu kwa undani mgogoro huo na baada ya kuelezwa sasa ataangalia cha kufanya.

Mchungaji huyo aliwaeleza waandishi wa habari jana (jumatano) kuwa Maalim Seif ni rafiki yake na alitaka kujua Profesa Ibrahim Lipumba (Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa) amepatwa na nini hadi akivuruge chama hicho.
Maalim Seif yeye amesema amezungumza kwa kina na Askofu Gwajima kuhusu  mgogoro wa CUF na amemuacha atafakari akiamini baada ya hapo huenda akafanya jambo.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: