Mjadala wa wagombea urais Kenya kufanyika Julai


9 Mei 2017


Mjadala wa urais nchini Kenya uliofanyika muda mfupi kabla ya uchaguzi wa mwaka 2013

Mjadala wa urais nchini kenya uliofanyika muda mfupi kabla ya uchaguzi wa mwaka 2013
Vyombo vya habari nchini Kenya vitaandaa mijadala mitatu ya wagombea urais mwezi mmoja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo.
Mijadala hiyo itafanyika tarehe tofauti za mwezi Julai.
Mjadala wa kwanza utakaokuwa wa urais utafanyika mnamo tarehe 10 mwezi Julai.
Ule wa manaibu wa rais utafanyika tarehe 17 huku mjadala wa tatu wa urais ukifanyika tarehe 24 mwezi Julai.
Mijadala yote itafanyika katika chuo kikuu cha Catholic University Afrika Mashariki kuanzia mwendo wa 7.30 usiku na itapeperushwa moja kwa moja na vyombo vyote vya habari katika runinga na redio.
Tangazo hilo lilifanywa siku ya Jumanne na Wachira Waruru ambaye ni mwenyekiti wa kamati andalizi.
Hii ni mara ya pili mjadala wa urais unafanyika nchini Kenya.
Mjadala wa kwanza ulifanyika kabla ya uchaguzi mkuu wa 2013.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: