Mamlaka ya afya katika mji mkuu wa Yemeni Sanaa, imetangaza hali ya hatari baada ya kutokea mlipuko wa kipindu pindu ambao umeua watu kadhaa.
Hospitali za mjini ambao unadhibitiwa na waasi wa Houthi zimejaa wagonjwa wa kipindu pindu.
Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limesema kuwa idadi ya wagonjwa inaongezeka mara tatu kila wiki kwa zaidi ya watu elfu nane.
Ugonjwa huo unasambaa kwa kasi nchini Yemeni ambayo pia inakabiliwa na baa la njaa sambamba na vita.
0 Post a Comment:
Post a Comment