Spika wa Bunge lenye wapinzani wengi nchini Venezuela, Julio Borges amelitaka jeshi la nchi hiyo kuanzisha mazungumzo na kusaidia kupata suluhu ya mgogoro wa kisiasa.
Jeshi linamtii rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro ambaye amekuwa akipinga shinikizo la upinzani kuitisha uchaguzi mapema.
Borges amemtaka waziri wa ulinzi, Vladmir Padrino Lopez, kukutana na viongozi wa upinzani na kusikiliza hoja zao.
Amesema jeshi halitakiwi kuegemea upande mmoja, kazi yake ni kutetea katiba ya Venezuela, ambayo upinzani inasema inatishiwa.
Mapema mwezi huu, Rais Maduro alitangaza mipango ya kuunda bunge jipya kwa ajili ya kuandika katiba mpya.
0 Post a Comment:
Post a Comment