Korea Kaskazini imesema zoezi la kujaribu makombora yake lilifanikiwa kwa asilimia 100 siku ya Jumapili.
Kombora hilo ni aina mpya yenye uwezo wa kubeba vilipuzi vingi zaidi.
Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vinasema jaribio hilo limeusisha kombora la masafa ya kati liitwalo Hwasong-Twelve.
Vinasema pia kuwa Rais wa nchi hiyo Kim Jong-Un alishuhudia moja kwa moja tukio hilo.
Marekani imetaka Korea Kaskazini kuwekewa vikwazo zaidi kwani inahatarisha usalama wa dunia.
0 Post a Comment:
Post a Comment