Wapiganaji wa Palestina Hamas wamepata kiongozi mpya.
Kiongozi huyo ni Ismail Haniyeh ambaye hadi hivi karibuni alikuwa ndio kiongozi wa kundi hilo katika ukanda wa Gaza.
Akijulikana kama kiongozi anayetumia akili nyingi wakati wa kutatua maswala, anachukua mahala pake Khaled Meshaal ambaye ameliongoza kundi hilo akiwa ughaibuni kwa miongo miwili.
Uchaguzi wa kiongozi mpya ulifanyika kupitia njia ya Video Link kati ya wajumbe waliopo katika ukanda wa Gaza na wale waliopo nchini Qatar ambako Meshaal ana makao yake.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa bwana Meshaal anaachia ngazi wakati ambapo Hamas limeanza kulegeza msimamo wa kisiasa.
Kwa mara ya kwanza wiki iliopita katika sera mpya kundi hilo liliwachilia wito wake wa kuiharibu Israel.
Hamas bado lina wapiganaji wake katika eneo la Gaza na bado linaaminika kuwa kundi la kigaidi na Israel Marekani na mataifa ya bara Ulaya.
0 Post a Comment:
Post a Comment