Umoja wa Mataifa umesema kuwa mashirika ya kutoa misaada ya kimataifa yamepunguza shughuli zake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kufuatia mashambulizi kadhaa dhidi ya wafanyakazi wao.
Mashirika manne ya kimataifa yamesitisha shughuli zake katika eneo la Ouham na Madkatari wasio na mipaka MSF wamesema kuwa wanawatibu wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura pekee.
Umoja wa Mataifa unakisia kuwa nusu ya raia wote wa CAR hutegemea chakula na madawa ya misaada kila siku.
Taifa hilo limevurugika kutokana na mapigano kati ya makundi mawili ambayo asili yake ni kundi la zamani la Kiislamu la Seleka, lililompindua Rais mwaka 2013.
0 Post a Comment:
Post a Comment