6 Mei 2017
Kamati ya kampeni ya mmoja wa mgombea wa urais nchini Ufaransa, Emmanuel Macron, imesema kuwa imevamiwa vikali na makundi ya udukuzi ambayo yamechapisha habari muhimu ya kundi lao katika mitandao ya kijamii.
Washiriki wa Bwana Macron wamesema kuwa barua pepe sahihi zimeibwa katika tarakilishi zao na kuchanganywa na zile bandia ili kuonyesha kuwa kamati hiyo ya Bwana Macron ni ya ubabaishaji tu.
Chama cha Bwana Macron kijulikanacho nchini kama "En Marche" kilisema kuwa wachapishaji wa habari hizo zilizovurugwa wana nia ya kuvuruga demokrasia kabla ya uchaguzi wa marudio ya hapo kesho.
Tume ya Uchaguzi nchini Ufaransa inatarajiwa kuongoza mkutano wa dharura baadaye hii leo kujadili madai hayo ya udukuzi.
0 Post a Comment:
Post a Comment