13 Mei 2017
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alitoa kauli hiyo jana bungeni ambapo alisema kuwa Jiji hilo limejengwa kwa Master Plan ya mwaka 1979.
“Tunachokifanya Dar es Salaam ni kurasimisha tu katika maeneo walikojenga wananchi ili hawa masikini wasipoteze haki yao na kikubwa tunachoangalia ni kupatikana kwa barabara lakini mji huo tutaupanga upya vizuri na kisasa,” alisema Lukuvi
Aliwataka wabunge wa Kibamba na Ubungo kuwa watulivu kwani tayari waziri huyo alishafanya kazi ya kupitia maeneo hayo wakishirikiana na mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea ambapo wananchi walikuwa wanatoa ushirikiano.
Awali, Mbunge wa Kibamba John Mnyika (Chadema) alitaka kujua ni maeneo gani ambayo hayajapimwa katika jimbo la Kibamba na yatapimwa lini.
“Je kuna mpango gani wa kupunguza gharama na muda wa upimaji na utoaji wa hati ili kurahisisha na kuharakisha upatikanaji wa huduma tajwa,” alihoji Mnyika
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo alimtaka mbunge huyo kuwa makini katika baraza la madiwani kwani ameuliza maswali ambayo alipaswa kuuliza akiwa katika baraza ambako yeye ni mjumbe.
“Tayari upimaji unaendelea katika Kata ya Kimara ambapo viwanja 3,196 vimepimwa, na taratibu zinakamilishwa kuwapimia wananchi 186 waliolipia gharama katika Kata ya Kibamba,” alisema Jafo
Alitaja viwango vya gharama za upimaji kuwa vipo kwa mujibu wa sheria ambavyo vilipangwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na kwa kuzingatia matumizi ya zana za kisasa.
Alisema matumizi ya mifumo hiyo yamerahisisha zaidi upimaji ambao ramani za hati (deed plan) katika Manispaa ya Ubungo zimeongezeka na kufikia hati 1,000 kwa mwezi.
0 Post a Comment:
Post a Comment