Mbaroni kwa kukutwa na fuvu la binadamu



Mganga wa kienyeji, Moshi Mohamed Matimbwa
Mganga wa kienyeji, Moshi Mohamed Matimbwa (26), (aliyevua shati) na msaidizi wake aliyetambulika kwa jina la Ally Omari Mapande (23) wakazi wa wilayani Kibiti wamekamatwa na Polisi baada ya kukutwa na fuvu la binadamu 
 Jeshi la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu wawili wakazi wa Kibiti kwa tuhuma za kukutwa na fuvu la kichwa cha  binadamu.
Akithibithisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani,  Onesmo Lyanga amesema watu hao walikamatwa  mwishoni mwa wiki iliyopita wakati polisi wakiwa kwenye doria katika kijiji ya Jaribu.
Lyanga amesema watuhumiwa hao waliokuwa wakitoka Mkuranga kuelekea Kibiti kwa kwa kutumia pikipiki  walikuwa wameficha fuvu hilo kwenye begi.
Amesema baada ya kufika katika kijiji hicho wakiwa kwenye pikipiki  walisimamishwa na polisi waliokuwa doria eneo hilo na baada kuwakagua ndipo walipokuta fuvu hilo ndani ya begi.
Amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini mahali lilipotoka fuvu hilo.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: