Akizungumzia kuhusu ujenzi huo Mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo, Hussein Gonga amesema ujenzi wa hospitali hiyo, utagharimu zaidi ya Sh200 milioni .
Gonga amesema ujenzi wa hospitali hiyo ukikamilika utawaondolea adha wananchi hasa wanawake na watoto wanaoishi kwenye vijiji vilivyopo maeneo hayo kero ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu.
Amesema kwa kushirikiana na wananchi na viongozi mbalimbali wa eneo hilo atahakikisha jengo hilo lina kamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma.
“Uamuzi wa kujenga jengo hili maalum ni moja ya mpango niliojiwekea mwaka huu ikiwamo kuokoa maisha ya mama na mtoto. Lakini pia kuhakikisha jamii inayozunguka mgodi huu inaendelea kunufaika kwa uwepo wa kituo hiki,” amesema Gonga.
Mhandisi anayesimamia ujenzi huo, Robert Mwanyika amesema ujenzi huo unatarajiwa kukamilika katika kipindi kisichozidi miezi mitatu.
0 Post a Comment:
Post a Comment