Mgahawa mmoja mjini London umekumbwa na habari bandia za kuuza nyama ya mtu.
Wafanyikazi katika mgahawa wa Karri Twist katika eneo la New Cross nchini Uingereza wamehangaishwa kwa kupigiwa simu kutoka kwa wateja wanaosema ''Kwa nini hamujafunga''?.
Mgahawa huo wa chakula cha jioni ni mwathiriwa wa habari za mzaha zilizodai kwamba mmiliki wake alikamatwa kwa kuweka nyama ya binadamu katika chakula na kwamba miili 9 ilipatikana katika jokovu la mgahawa huo.
Na watu wengine waliamini mzaha huo.
Habari hiyo ilichapishwa katika chombo cha habari cha channel23news.com, mtandao ambao wateja wake wanaweza kuchapisha habari za uwongo ili kuwafanyia mzaha rafiki zao kwa kuchapisha moja kwa moja katika mtandao wa fecbook.
Shinra Begum ambaye ndio mmiliki wake aliambia Newsbeat kwamba biashara hiyo ya familia imekumbwa na wakati mgumu tangu habari hiyo ilipochapishwa siku ya Alhamisi.
''Wakati watu walipoanza kunipigia simu na kuuliza iwapo tulikuwa tukiuza nyama ya binadamu sikuamini''.
''Nilishtuka nilipoaana habari hiyo katika mtandao na kuendelea kusambazwa katika mtandao wa facebook''.
Sasa watu wametishia kulivunja jengo letu na nimelazimika kuketi chini na mteja ili kumuelezea kwamba yote hayo ni madai ya uwongo.
Shinra anasema kuwa alilazimika kuripoti kwa maafisa wa polisi kwa sababu lilikuwa swala lililomtia wasiwasi mkubwa.
Njia ya pekee ambapo Karri Twist iliweza kukabiliana na chuki hiyo ni kupitia kuchapisha katika mtandao wao ili kuhakikisha kwamba watu wanajua kwamba hilo halikuwa la kweli.
0 Post a Comment:
Post a Comment