Trump amekiri kukerwa na tuhuma hizi
Chama cha Democrat kimesema Rais Donald Trump anapaswa kuruhusu uchunguzi huru kufanyika kuhusu tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi uliopita wa Marekani kama kweli hakuhusika.
Kiongozi mkuu wa chama cha Democrat katika bunge la Marekani Nancy Pelosi amesema jambo hilo litaondoa mashaka ambayo yapo miongoni mwa wengi.
Mkuu wa zamani wa FBI Robert Mueller ameteuliwa kuongoza uchunguzi huo,lakini Pelosi anasema bado atasimamiwa na uongozi wa Trump.
Rais Trump amesema kwamba ameingia katika vita kubwa katika historia ya siasa ya za Marekani
0 Post a Comment:
Post a Comment