Michelle Obama aukosoa utawala wa Trump


13 Mei 2017


Michelle Obama aukosoa utawala wa Trump
Haki miliki ya pich
Michelle Obama ametetea vikali mipango ya kuwapatia wanafunzi vyakula bora vyenye afya alivyopigania akiwa m,ke wa rais.
Katika kongamano la afya mjini Washington ,aliushutumu uongozi wa rais Trump kwa kufutilia mbali viwango vya lishe bora inayolenga kuwafanya wanafunzi kuwa wenye afya nzuri.
''Sijui kwa nini mtu anapendelea watoto kula vyakula visivyo bora'' ,alisema.
Mmoja kati ya watoto watano nchini Marekani wanaugua ugonjwa wa kunenepa kupita kiasi, kulingana na takwimu za serikali.
Akikosoa sera za utawala wa rais Trump, bi Obama aliwaambia waliohudhuria kongamano hilo: Hapa ndipo unafaa kuangazia kuhusu malengo ya mtu.
Michelle Obama amekuwa akipigania watoto kuwa na lishe bora ili kukabiliana na tatizo la kunenepa kupitia kiasi miongoni mwa watoto Michelle Obama amekuwa akipigania watoto kuwa na lishe bora ili kukabiliana na tatizo la kunenepa kupita kiasi miongoni mwa watoto
Lazima ujiulize kwa nini hutaki watoto wetu kula vyakula vyenye lishe bora katika shule? Na ni kwa nini hilo liwe tatizo, kwa nini hilo liingiziwe siasa? Kunaendelea nini jamani?Aliongezea: Musinishirikishe mahala popote: nipende usinipende, fikiria kwa nini mtu anapendelea mtoto wako kula chakula kibaya.
Kwa nini usherehekee, Kwa nini ufurahie kitu kama hicho? Kwa sababu hii hapa siri: Iwapo mtu anafanya hivyo hawatilii maanani watoto wenu.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: