Mkuu wa benki wa Yahya Jammeh afutwa kazi Gambia


10 Mei 2017

Rais Barrow amekuwa akiwafuta kazi maafisa wakuu waliokuwa wa Rais Jammeh

Haki miliki ya picha
Rais Barrow amekuwa akiwafuta kazi maafisa wakuu waliokuwa wa rais Jammeh
Mkuu wa Benki Kuu ya Gambia aliyekuwa akihudumu wakati wa utawala wa Yahya Jammeh, Amadou Colley, amefutwa kazi.
Hakuna sababu zozote zilizotolewa kuhusiana na kufutwa kwake.
Bw Colley mwenyewe ameambia Reuters kwamba hajui ni kwa nini ameachishwa kazi.
"Tulipokea barua leo, ambazo hazikueleza sababu ya kufutwa kazi kwetu. Zilisema tu kwamba 'Huduma zenu hazihitajiki tena,'" alisema.
Bw Colley alihudumu chini ya Rais Jammed ambaye alituhumiwa na baadhi ya maafisa wa serikali mpya kwamba alipora mamilioni ya dola kutoka kwa hazina ya serikali wakati wa utawala wake wa miaka 22.
Tangu achukue madaraka Januari, Rais Adama barrow amekuwa akiwafuta kazi na kuteua maafisa wapya katika nyadhifa zenye ushawishi serikalini.
Bw Barrow alimshinda Jamme kwenye uchaguzi mkuu Desemba, ingawa rais huyo alikubali kuondoka wiki kadha baadaye baada ya kushinikizwa na jamii ya kimataifa.
Kwa sasa, Jammeh anaishi uhamishoni Equatorial Guinea.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: