Msichana wa Chibok akataa kurudi nyumbani


10 Mei 2017

Wazazi wanasubiri kujuaiwapo baadhi ya wasichana walioachwa ni wana wao
Wasichana wa Chibok
Haki miliki ya picha
Mmoja wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua kusalia na mumewe badala ya kuachiliwa huru kulingana na msemaji wa rais wa Nigeria.
Alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la wasichana walioachiliwa siku ya Jumamosi.
Garba Shehu aliambia runinga moja kwamba wasichana 83 walitarajiwa kuachiliwa huru lakini mmoja wao akasema : hapana nafurahi nilipo, nimepata mume.
Wasichana 82 waliachiliwa huru ikiwa ni kati ya mazungumzo yalioafikiwa na shirika la ICRC.
Serikali ilikubali kuwaachilia huru wanachama wanne wa Boko haram kubadilishana na uhuru wa wasichana hao .
.Haki miliki ya 
Wapganaji hao wanadaiwa kuwazuilia zaidi ya wasichana 100 kati ya 276 waliowateka katika eneo la Chibok miaka mitatu iliopita.
Kundi hilo pia limewateka maelfu ya raia wakati wa operesheni zao katika eneo hilo.
Inaaminika kwamba baadhi ya wale waliotekwa wameozwa wapiganaji na wamepata watoto nao.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: