Muhongo avuliwa Uwaziri wa nishati na madini


25 Mei 2017



Profesa Sospeter Muhongo
Profesa  Sospeter Muhongo

 Rais John Magufuli amemuondoa Profesa Sospeter Muhongo kwenye Baraza la Mawaziri katika sakata la mchanga wa dhahabu, lakini inaonekana haikuwa kazi rahisi kwake.
Hii ni mara ya pili kwa Profesa Muhongo kuachia uwaziri huo nyeti ndani ya miaka minne, anaingia katika orodha ya mawaziri wengi wa nishati na madini waliolazimika kujiuzulu au uteuzi wao kutenguliwa.
Jana, mambo matatu yalijitokeza kwa Magufuli; alikuwa akitengua uteuzi wa waziri wa tatu tangu aunde Serikali ya Awamu ya Tano, alikuwa anamuondoa “rafiki” yake na alikuwa akimuondoa mtu ambaye hakuwahi kuona mwingine anayefaa Wizara ya Nishati na Madini zaidi yake.
Na mtiririko wa kutangaza hatua alizochukua kwa haraka baada ya kukabidhiwa ripoti ya kamati iliyochunguza sakata la kiwango cha madini kwenye makontena ulionyesha ugumu huo kwani jina la Profesa Muhongo lilikuwa la mwisho.
Rais aliunda kamati hiyo kuchunguza madini yaliyomo katika makontena 277 ya mchanga yaliyokuwa yakisafirishwa kwenda nje ya nchi kuyeyushwa kupata masalia baada ya mchakato wa kwanza wa kuondoa dhahabu mgodini.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: