7 Mei 2017
Korea Kaskazini inasema kuwa imemkamata raia wa Marekani kwa kushukiwa kuendesha vitendo viovu dhidi ya taifa hilo.
Kim Hak-song, alikuwa akifanya kazi katika chuo cha sayansi na Teknolojia cha Pyongyang PUST na alikamatwa jana Jumamosi
Raia wengine watatu wa Marekani kwa sasa wanazuiliwa nchini Korea Kaskazini akiwemo Kim Sang-duck, ambaye alikuwa mhadhiri katika chuo cha PUST
Awali Marekani iliilaumu Korea Kaskazini kwa kuwakamata raia wake kuwatumia kwa udhamini.
Kukamatwa mtu huyo kunakuja huku kukishuhudiwa msukosuko kati ya Korea Kaskazini na Marekani.
Korea Kaskazini imetisha kufanya majaribio ya kombora la nuklia huku Marekani nayo ikituma meli ya kivita eneo hilo kuizuia Korea Kaskazini kuunda zana za nuklia.
Kim Hak-song ndiye raia wa nne wa Marekani kukamatwa nchini Korea Kaskazini.
0 Post a Comment:
Post a Comment