Rais Zuma azuiwa kutoa hotuba Afrika Kusini


  • 1 Mei 2017
Bwana Zuma ameapa kusalia ofisini hadi muhula wake ukamilike mwaka 2019
 Bwana Zuma ameapa kusalia ofisini hadi muhula wake ukamilike mwaka 2019
Rais wa Afrika Kusini anayekumbwa na kashfa Jacob Zuma, ameondoka kwenye mkutano wa siku ya kimataifa ya wafanyazi baada ya kukemewa na wafanyakazi wanaomtaka ajiuzulu.
Fujo zilizuka kati ya wafuasi wa Bwana Zuma na wapinzani na kusabababisha hotuba yake kufutwa.
Chama kikuu cha wafanya kazi Cosatu, kilimtaka Bwana Zuma ajiuzulu mwezi uliopita baada ya kumfuta kazi waziri wa fedha alijekuwa akiheshimiwa sana.
Bwana Zuma ameapa kusalia ofisini hadi muhula wake ukamilike mwaka 2019.
Maandamano yamekuwa yakifanyika kumtaka Zuma ajiuzuluHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaandamano yamekuwa yakifanyika kumtaka Zuma ajiuzulu
Alionyeshwa na runinga akiondoka jukwaani kwa hasira na kuondolewa na magari kutoka kwa mkutano ulioandaliwa mjini Bloemfontein
Maafisa wa vyeo vya juu wa ANC nao walikemewa kwenye mkutano uliofanyika mjini Durban.
Shinikizo za kumtaka Zuma ajiuzulu zimekuwa zikoongezeka tangu amfute kazi waziri wa fedha Pravin Gordan mwezi Machi.
 Mshirikishe Mwenzako: zakacheka.blogspot.com/ www.zakacheka.simplesite.com +255 625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: