Wasiwasi wa Marekani kujiondoa kwenye makubaliano ya mazingira


 9 Mei 2017


Trump anaamini kuwa sheria zamazingira zitakuwa na athari kwa uchimbaji wa makaa ya mawe, mafuta na gesi.
Wapatanishi wa mazingira wanaokutana mjini Bonn wameanza kazi licha na wasiwasi wa kundelea kushiriki kwa Marekani siku zinazokuja.
Mazungumzo haya yana lengo la kuweka sheria za kutekelezwa wa makubaliano yaliyotiwa sahihi mjini Paris mwaka 2015.
Lakini kuna hofu kuwa huenda Rais Trump akajiondoa kutoka kwa makubaliano ya kihistoria.
Baadhi ya wajumbe wanasema kuwa hatua kama hiyo itakuw ni pigo kwa makabaliano hayo.
Mkutano huu wa Mei unaoandaliwa katika makao ya Umoja wa Mataifa haukui na shughuli nyingi lakini huu ndio wa kwanzawa wajumbe tangu Donald Trump aapishwe.
Waandamanaji wanaopinga mipango ya mazingira ya Rais Trump
Waandamanaji wanaopinga mipango ya mazingira ya rais Trump
Wengi wanahofu kuwa itakuwa mara ya kwanza rais huyo mpya kuamua kuondoa ushiriki wa Marekani katika makubaliano ya Paris.
Wakati wa kampeni rais Trump alikosoa makubaliano hayo ya Paris. Alisema angefuta makubaliano ambayo yameafikiwa na nchi 140 na kuanza kutekelezwa rasmi mwezi Novemba mwaka uliopita.
Trump amekuwa na wasiwasi wa kuondolewa kwa sheria za mazingira ambazo anaamini kuwa zitakuwa na athari kwa uchimbaji wa makaa ya mawe, mafuta na gesi.
Wachanganusi wengi wanaamini kukwa Bwana Trump ameanza kusikiliza watu wakiwemo waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Rex Tillerson, ambaye anataka Marekani kusalia kwenye makubaliano hayo akidai kuwa ni muhimu Marekani kuwa na nafasi katika makubaliano hayo.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: