James Comey: Utawala wa Trump ulisema "uongo mtupu" kuhusu mimi na FBI.


9 Juni 2017

Former FBI director James Comey
Comey amesema alikanganyikiwa na sababu zilizotolewa kuhusu kufutwa kazi kwake
Aliyekuwa mkuu wa Shirika la uchunguzi wa jinai la Marekani FBI James Comey ameambia Bunge la Congress kwamba utawala wa Trump ulisema "uongo mtupu" kumhusu yeye na FBI.
Bw Comey ameambhia kamati ya Seneti kwamba walikosea kukosoa shirika hilo na uongozi wake.
Alisema pia kwamba alikanganywa na kubadilishwa kwa taarifa kuhusu kilichosababisha kufutwa kazi kwake, ambako kulitokea baada yake kuongoza uchunguzi kuhusu uwezekano wa kuwepo uhusiano kati ya maafisa wa kampeni wa Bw Trump na Urusi.
Bw Comey alisema kwamba Bw Trump alimweleza mara nyingi kwamba alikuwa akifanya "kazi nzuri sana".
Lakini alisema anafahamu kwamba rais ana haki ya kumfuta mkuu wa FBI wakati wowote ule.
Mkuu huyo wa zamani wa FBI alikuwa ametulia kipindi chote cha saa mbili alipokuwa anatoa ushahidi, lakini alionekana kutekwa na hisia alipokuwa anaanza kuzungumza.
Aliambia kikao hicho cha Maseneta kwamba White House "waliamua kuniharibia jina, na zaidi FBI" kwa kudai kwamba shirika hilo lilikuwa "linaongozwa vibaya".
"Uliokuwa ni uongo mtupu. Ninasikitika sana kwamba wafanyakazi wote wa FBI walisikia hayo," aliendelea.
"FBI ni shirika lenye ukweli. FBI ni thabiti. Na FBI ni na itaendelea kuwa huru," alisema akianza kuzungumza.
Bw Comey alikuwa anaongoza uchunguzi kuhusu Urusi kabla ya Bw Trump kumfuta kazi.
Mashirika ya ujasusi ya Marekani yanaamini kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani na wanachunguza uhusiano kati ya maafisa wa kampeni wa Bw Trump na Urusi.
Comey akila kiapo
Comey akila kiapo
Lakini kufikia sasa hakujapatikana ushahidi wowote wa kuthibitisha kushiriki kwa maafisa wa Urusi.
Bw Trump amekuwa akipuuzilia mbali taarifa hizo kama "habari za uongo".
Bw Comey, akihutubu Alhamisi, alisisitiza kwamba uwezekano kwamba Urusi iliingilia uchaguzi huo haukuwa "jambo la kubahatisha" na kuongheza kwamba: "Hakufai kuwa na shaka kuhusu hilo."
Alipouliwa na kamati hiyo iwapo rais huyo alijaribu kusitisha uchunguzi kuhusu madai ya kuhusika kwa Urusi, Bw Comey alisema: "Sina habari kuhusu hilo, hapana."
Alisema pia kwamba si wajibu wake kubaini iwapo vitendo vya Bw Trump vilikuwa sana na kuingilia utekelezaji wa haki.


Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: