Watu 10,000 waukimbia moto Afrika Kusini


9 Juni 2017

Property on fire
Nyumba zaidi ya 150 zimeteketea katika mtaa wa Knysna

Fires
Knysna ni maarufu sana kwa watalii
Watu takriban 10,000 walilazimika kukimbia makwao kutoka mji mmoja pwani ya Afrika Kusini ambao umeharibiwa pakubwa na moto.
Wanajeshi wanashiriki katika juhudi za kukabiliana na mtaa huo kukabili moto huo ambao ulinawaka katika maeneo 25 katika mji wa Knysna.
Watu wanane walifariki kutokana na upepo mkubwa na moto ambao ulikumba mji huo na maeneo mengine katika kanda ya Cape Magharibi.
Upepo huo mkubwa ulisaidia kueneza moto huo.
Nyumba zaidi ya 150 ziliteketezwa eneo hilo kwa mujibu wa shirika la wazimamoto.
Mji huo una takriban wakazi 77,000.
Unapatikana kilomita 500 mashariki mwa mji wa Cape Town.
Jeshi la Taifa la Afrika Kusini lilisaidia kuangusha mabomu ya maji yanayotumiwa kuzima moto kusaidia kukabili moto huo, msemaji wa jeshi Simphiwe Dlamini amesema.
Wanajeshi karibu 150 walitumwa eneo hilo kuzuia wahalifu kupora mali katika maeneo ambayo wenyewe walikimbia.
Mwezi Mei, mkoa wa Cape Magharibi ulitangaza janga ya ukame baada ya mabwawa mawili makubwa kukauka kabisa.
Ukame huo unadaiwa kuwa mbaya zaidi kukumba eneo hilo katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja.
Mataifa mengine Afrika kusini yamekabiliwa an ukame wa zaidi ya miaka miwili, unaotokana na hali ya hewa ya El Nino.
Hata hivyo, maeneo mengine yamepata mvua kwa wingi na mavuno ya mahindi kuongezeka.


Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: