Kundi la wapiganaji wa Al -Shabab limewauwa askari 61 Somalia


8 Juni 2017

Wanajeshi 61 wahofiwa kuuwa na Al-Shabaab Puntland, SomaliaLicha ya kundi la Al-Shabab kulemewa, bado linadhibiti baadhi ya maeneo nchini Somali
Kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Al -Shabab
Kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Al -Shabab, linasema kuwa limewauwa askari 61 katika kambi moja ya kijeshi kaskazini mashariki mwa Bosaso nchini Somalia.
Kambi hiyo ya kijeshi ipo katika eneo la jimbo lililojitangazia uhuru wake la Puntland.
Utawala huko Puntland umethibitisha kutokea kwa shambulio hilo lakini unapinga idadi ya waliouwawa.
Duru zasema kuwa shambulio hilo la mapema Alhamisi asubuhi, lilitokea karibu na milima ya Galgala, ambao hapo awali ilikuwa ngome ya wapiganaji wa al-Shabab katika jimbo hilo la Puntland.
Kufikia sasa, bado hakujatolewa idadi rasmi ya waliouwawa, lakini waziri wa ulinzi wa Abdiaziz Hirsi amekanusha madai ya al-Shabab.
Haki miliki ya p
Anasema kuwa mamlaka inaendelea kuchunguza swala hilo na itatoa taarifa ya kina muda mfupi baadaye.
Jimbo la Puntland limekuwa likikumbwa na mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa al-Shabab, lakini hili la sasa limetajwa kuwa baya zaidi katika siku za hivi karibuni.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: