15 Juni 2017
Rais John Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana (Jumatano) na Profesa Adolf Mkenda, Katibu Mkuu, Biashara na Uwekezaji, imesema uteuzi huo umeanza Mei 31.
Baada ya uteuzi huo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewateua wajumbe sita wa bodi hiyo.
Wateule hao ambao uteuzi wao umeanza Mei 31 ni Profesa Winester Anderson, Dk Khatib Kazungu, Godfrey Simbeye, Dk Tausi Kida, Seif A. Seif na Mhandisi Peter Chisawilo.
0 Post a Comment:
Post a Comment