Melania Trump na mwanawe Baron wahamia White House


13 Juni 2017

Barron, Melania and Donald Trump arrive at the White House, 11 June
Melania Trump na mwanawe Baron wahamia White House
Melania Trump na mtoto wale wamehamia Ikulu ya Marekani ya White House miezi matano tangu mumewe Donald Trump kuingia ofisini
Bi Trump na mtoto wake kiume wa umri wa miaka 11 Baron, walikuwa wamebaki mjini New York ili kumuwezesha kumaliza masomo ya mwaka.
Hatua hiyo imekuwa ya kushangaza kwa wengi kwa kuwa ndiyo familia ya kwanza miaka ya hivi karibuni kukosa kuhamia Ikulu ya White House mara moja.
Mtangulizi wake Michelle Obama hata alhamia White House, mapema kuwezesha watoto wake kujunga na shule mapema.
Hata hivyo inaonekana kuwa Melania amefurahishwa na hatua yake kuhamia White House baada ya kuandika kwenye Twitter alipowasili.
Barron amekuwa akisomea shule ya kibinafsi iliyopo jiji la New York.
Trump si rais wa kwanza wa Marekani hivi karibuni kuhamia White House akiwa na watoto wa umri wa kwenda shule.
Rais Barack Obama alipoingia madarakani, mabinti wake Malia na Sasha walikuwa na umri wa miaka 10 na 7.
Rais Bill Clinton alipohamia ikulu Washington, Chelsea Clinton alikuwa na miaka 12.
Watoto hao wote walihamia White House masomo ya kiendelea na walihudhuria masomo shule ya Sidwell Friends, shule ya kibinafsi iliyo kaskazini magharibi mwa Washington.
A tweet from Melania Trump's @FLOTUS account, saying
Melania alipakia picha hii kwenye Twitter baada ya kuingia ikulu
Habari kwamba Melania na Barron hawangejiunga na Trump ikulu ya White House Januari ziliwashangazaa baadhi ya Wamarekani lakini pia zilisifiwa na baadhi wanaosema ni vyema kuweka mbele maslahi ya mtoto na malezi yake.
Msemaji wa shughuli ya mpito Jason Miller wakati huo alisisitiza kwamba Trump na familia yake wako tayari kutumikia Wamarekani na kwamba ni sababu ya mtoto pekee iliyomfanya kutohamia mara moja ikulu ya White House.
"Familia ya Kwanza huishi White House kama ishara muhimu kwa taifa letu na kwa ulimwengu wote," aliandika Pamela Benbow, mmoja wa watu kwenye Twitter. "Uamuzi wa Melania Trump unashangaza."
Wengi walilifanyia mzaha suala hilo wakisema ladha ya Bi Trump kuhusu mapambo ya nyumba ndiyo iliyomfanya kutotaka kuingia White House haraka.
Kunao pia waliodai hiyo ni ishara huenda mambo si mazuri katika ndoa yake na Bw Trump.
Wake wa Rais wa Marekani ambao hawakukaa White House wakati wa uongozi wa waume zao ni wawili pekee; Martha Washington, kwa sababu ikulu hiyo haikuwa imejengwa, na Anna Harrison, kwa sababu mumewe alifariki kabla ya kuhamia ikulu.
Wapo waliomuunga mkono Bi Trump.
"Vyema sana, hili ndilo jambo watoto wawajibikaji wanafaa kufanya kwa ajili ya mtoto wa umri wa Barron," mtu mwingine kwenye Twitter aliandika.
Si jambo la ajabu kwa Bi Trump kusisitiza umuhimu wa kumlea Barron. Wakati wa kampeni, mara kwa mara alikaa nyumbani kumtunza.
Marais wengine walifanya nini?

Bill Clinton, Hillary Clinton na Chelsea wakiwasili White House mjini Washington
Chelsea Clinton, na wazazi wake katika uwanja wa nyasi wa White House. Alisema baadaye kwamba maisha yake ya utotoni yalikuwa ya kawaida
William Seale, mwanahistoria katika Chama cha Historia ya White House ambaye pia ni mwandishi wa kitabu cha The President's House (Nyumba ya Rais), anasema mke wa Rais Grover Cleveland, Frances Folsom Cleveland, aliishi tu White House msimu wa sherehe na hafla nyingi rasmi.
Rais huyo alinunua nyumba muhula wake wa kwanza ambapo Bi Cleveland alikaa mara nyingi. Alizoea kuita nyumba yake "Oak View" ingawa ilijulikana sana kama "Red Top" kwa sababu ya paa jekundu.
Lakini mke huyo, aliyekuwa na miaka 21 alipoolewa na rais huyo wa miaka 49, alikuwa mwanamke wa kwanza kuolewa akiwa anaishi White House.
Bw Seale anasema suala la watoto kusubiri hadi wamalize mwako wa masomo shuleni lilikuwa la kawaida na halijamshangaza.
Anasema watoto wa Rais John Tyler, aliyemrithi William Henry Harrison baada ya kifo chake, hawakuhamia ikulu mara moja.
Mke wa James Madison, Dolley Madison, pia alimwachilia mwanawe kutoka kwa ndoa yake ya awali, Payne Todd, aendelee na masomo.
Kumekuwa na makundi mawili ya watoto wa umri wa kwenda shuleni White House miongo mitatu iliyopita: Chelsea Clinton, alikuwa na miaka 12 wakati huo, na Malia na Sasha Obama, waliokuwa na miaka 10 na saba mtawalia.
Walisafiri na wazazi wao baba zao walipoingia madarakani - lakini wote waliishi ikulu ya White House, katika barabara ya 1600 Pennsylvania Avenue tangu siku ya kuapishwa kwa baba zao.
Familia ya Obama ilipunguza tatizo hilo kwa kuwafanya mabinti wake wabadilishe shule mapema kwa kuhamia Washington mapema, wakati wa mapumziko mafupi, na wakaanza shule wiki chache kabla ya baba yao kuapishwa Januari 2009.
Obama na mabinti wake


Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: