Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wabunge wa kamati ya kupambana na rushwa (APNAC).
Mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa African Dream chini ya ufadhiri wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, (UNDP) kwa lengo la kuwajengea uwezo wabunge ili kupambana na tatizo hilo ambalo linaendelea kuwa mwiba mchungu kwa serikali.
Majawali amesema kwa sasa serikali imeamua kwa makusudi mazima kupambana na tatizo hilo na inafanya hivyo kwa kujua bado mchango wa taasisi nyingine unahitaji kumaliza jambo hilo.
“Maeneo ambayo bado kuna tatizo ni eneo la uchukuzi, Maji pamoja na polisi ambako bado kuna malalamiko kutoka kwa wananchi na lazima kuendelea kumulika maeneo hayo,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa
Hata hivyo amesema mkakati wa serikali ni pamoja na kuziomba mamlaka zinazohusika ikiwammo mahakama kuendesha kesi zote zinazohusiana na rushwa kwa haraka zaidi na kutoa hukumu ili pale inapobidi wahusika wachukuliwe hatua stahiki.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, serikali imeokoa kiasi cha Sh 53.9 bilioni tangu kuanza rasmi kwa mkakati wa mapambano hayo 2015/16 na wanaendelea kufanya mkakati wa kuzuia siyo kukamata.
0 Post a Comment:
Post a Comment