Tetemeko kubwa la ardhi latikisa Uturuki na Ugiriki


13 Juni 2017

Vifusi vya majumba yaliyoharibiwa na tetemeko mjini Plomari, Ugiriki
Vifusi vya majumba yaliyoharibiwa na tetemeko mjini Plomari, Ugiriki
Tetemeko kubwa la ardhi limetokea katika pwani ya Aegean maeneo ya magharibi mwa Uturuki na kuathiri pia visiwa vya Lesbos nchini Ugiriki.
Mitetemeko ya ardhi ilisikika pia Istanbul na Athens.
Kitovu cha tetemeko hilo la nguvu ya 6.3 kwenye vipimo vya Richter kilimuwa kilomita tano kusini mwa mji wa Plomari nchini Ugiriki, kusini mwa Lesbos, Idara ya Utafiti wa Jiolojia ya Marekani imesema.
Nyumba kadha ziliharibiwa, meya ya mji huo alisema.
Hakujatolewa taarifa zozote za majeruhi kufikia sasa.
Uturuki na Ugiriki huwa kwenye eneo lenye nyufa na mitetemeko ya ardhi hutokea mara kwa mara.
"Tumeizoea mitetemeko sisi kama watu wa Izmir lakini hili lilikuwa tofauti. Nilidhani mwenyewe kwamba wakati huu tungefariki dunia," Didem Eris, daktari wa meno wa umri wa miaka 50 anayeishi mji wa Izmir pwani ya Uturuki aliambia Reuters.
Watu wakiwa barabarani baada ya kuambiwa waondoke kwenye nyumba zao Izmir, magharibi mwa Uturuki
Watu wakiwa barabarani baada ya kuambiwa waondoke kwenye nyumba zao Izmir, magharibi mwa Uturuki
Uturuki na Ugiriki zimekumbwa na mitetemeko mingi ya ardhi miaka ya karibuni.
Watu zaidi ya 51 walifariki baada ya tetemeko ya nguvu ya 6.0 kutikisa mashariki mwa Uturuki Machi 2010.
Mwaka 1999, tetemeko la nguvu ya 7.6 lilitikisa mji wa Izmit na kuua zaidi ya watu 17,000 na kuacha karibu watu nusu milioni wakiwa bila makao kaskazini magharibi mwa Uturuki.
 Bonyeza hapa kwa habari zingine: zakacheka.blogspot.com  +255 625966236

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: