Urusi imeonya kuwa itashambulia ndege za muungano unaoongozwa na Marekani



19 Juni 2017

Ndege aina ya F/A-18E Super Hornet (sawa na iliyo pichani) ilitungua ndege ya serikali ya Syria
Ndege aina ya F/A-18E Super Hornet (sawa na iliyo pichani) ilitungua ndege ya serikali ya Syria
Urusi imeonya kuwa itashambulia ndege za muungano unaoongozwa na Marekani nchini Syria iwapo ndege hizo zitapaa katika maeneo ambayo jeshi lake linahudumu.
Hii ni baada ya ndege ya kivita ya Marekani kutungua ndege ya kivita ya serikali ya Syria.
Muungano huo unaoongozwa na Marekani ulisema ndege moja yake ilitungua ndege ya Syria aina ya Su-22 baada ya ndege hiyo kuangushia mabomu wapiganaji wanaoungwa mkono na Marekani katika mkoa wa Raqqa, Jumapili.
Urusi, mshirika mkuu wa serikali ya Syria, imesema pia kwamba itakatiza mawasiliano yote na Marekani ambayo lengo lake huwa kuzuia ajali angani.
Syria imeshutumu shambulio hilo la Marekani na kusema litasababisha "matokeo mabaya sana".
Urusi imejibu vipi?
"Ndege yoyote, ikiwa ni pamoja na ndege za kawaida na ndege zisizokuwa na rubani ambazo ni za muungano wa kimataifa unaohudumu magharibi mwa mto Euphrates, zitafuatiliwa na majeshi ya kukabiliana na ndege angani na ardhini na zitachukuliwa kama kitu kinachofaa kushambuliwa," wizara ya ulinzi ya Marekani imesema.
Urusi imekanusha madai kwamba Marekani ilikuwa imewasiliana na maafisa wa urusi kabla ya ndege hiyo aina ya Su-22 kutunguliwa.
Maafikiano kati ya Urusi na majeshi ya muungano unaoongozwa na Marekani ya kushirikiana kuzuia ajali angani na pia kuhakikisha usalama yalifika kikomo Jumatatu, wizara hiyo iliongeza.
Hii si mara ya kwanza mawasiliano kusitishwa kati ya pande hizo mbili.
Aprili, mawasiliano yalisitishwa baada ya Marekani kurusha makombora aina ya 59 Tomahawk katika kambi ya ndege za kijeshi ya Shayrat, nchini Syria.
Marekani ilishambulia baada ya Syria kudaiwa kutekeleza shambulio la kemikali katika maeneo yaliyoshikiliwa na waasi katika mkoa wa Idlib.
Lakini mataifa hayo mawili yalifufua mawasiliano yao mwezi uliopita.

F/A-18E Super Hornet
Ndege aina ya F/A-18E ikiwa angani

Haki miliki ya pich
Marekani imejitetea
Ndege hiyo ya kivita ya Syria aina ya Su-22 ilitunguliwa na F/A-18E Super Hornet karibu na mji wa Tabqa mkoa wa Raqqa Jumapili alasiri, wizara ya ulinzi ya Marekani imesema.
Inaaminika kwamba ndicho kisa cha kwanza kabisa cha ndege yenye rubani ya Marekani kutungua ndege nyingine ya kivita yenye rubani tangu vita vya Kosovo mwaka 1999.
Waasi wa Syrian Democratic Forces (SDF) wanaoungwa mkono na Marekani, na ambao wanakabiliana na wapiganaji wa Islamic State kama sehemu ya kampnei kubwa ya kuwafurusha IS kutoka mji wa Raqqa, wamekuwa wakihudumu eneo la Tabqa.
Taarifa ya muungano huo unaoongozwa na Marekani, ambao hufahamika kama Operation Inherent Resolve, imesema wapiganaji wanaoungwa mkono na serikali walishambuliwa wapiganaji wa SDF na kuwafurusha kutoka mji wa Ja'Din.
Majeshi ya muungano huo unaoongozwa na Marekani yanasema yalifanya operesheni ya kudhihirisha nguvu zake angani, kwa kutuma ndege za kivita kutishia ndege hizo za kivita za Syria ili kuzuia shambulio hilo. Kisha, wanasema waliwasiliana na Urusi kujaribu kuzuia hali isiwe mbaya.
Hata hivyo, wanasema ndege hiyo aina ya Su-22 iliangusha mabomu kwenye maeneo yenye wapiganaji wa SDF saa chache baadaye, na wanajeshi hao wa muungano wanasema kwa kufuata sheria za vita na haki ya kujilinda, walitungua ndege hiyo mara moja.
Juhudi za kuitahadharisha ndege hiyo kupitia mawasiliano ya masafa ya redio ya dharura zilifeli, wakuu wa majeshi ya Marekani wamesema.
Majeshi ya Urusi na Marekani yanasema ndege hiyo ilikuwa imeenda kushambulia wapiganaji wa IS, kilomita 40 kusini magharibi mwa Raqqa, iliposhambuliwa.
Jeshi la Syria limesema kisa hicho kinaweza kuwa na "madhara makubwa" katika vita dhidi ya ugaidi.
Urusi imesema kupitia taarifa yake kwamba rubani wa ndege hiyo ya Syria alifanikiwa kutoka kwenye ndege hito lakini alikuwa eneo linalodhibitiwa na IS na "hatima yake haijulikani".

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: