Urusi: Marekani imetangaza ''vita vya kibiashara'' dhidi yetu

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM

3 Agosti 2017
Putin na Trump: Waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev amesema kuwa vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa hilo ni sawa na kutangaza vita vya kibiashara.
Putin na Trump: Waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev amesema kuwa vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa hilo ni sawa na kutangaza vita vya kibiashara.
Waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev amesema kuwa vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa hilo ni sawa na kutangaza vita vya kibiashara.
Amesema kuwa mikakati iliotiwa saini na rais Trump inaonyesha udhaifu wa rais huyo wa Marekani ambaye alisema ameaibishwa na bunge la Congress.
Sheria hiyo inalenga kuiadhibu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani wa 2016 pamoja na vitendo vyake dhidi ya Ukraine.
Bwana Trump alilishutumu bunge la Congress kwa kupindua sheria.
Katika kutia saini makubaliano hayo dhidi ya adui wa Marekani kupitia sheria ya vikwazo siku ya Jumatano, aliweka taarifa akisema kuwa mkakati huo sio wa sawa.
Sheria hiyo pia inaiwekea vikwazo Iran na Korea Kaskazini.
Iran imesema kuwa vikwazo hivyo vipya vinakiuka makubaliano ya mpango wa nyuklia na kwamba itajibu kwa njia ilio ''sahihi na sawia'' kulingana na chombo cha habari cha Isna.
Waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev amesema kuwa vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa hilo ni sawa na kutangaza vita vya kibiashara.
Waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev amesema kuwa vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa hilo ni sawa na kutangaza vita vya kibiashara.

Haki miliki ya pichKorea Kaskazini kwa upande wake haijatoa matamshi yoyote kuhusiana na hatua hiyo ya Marekani.
Bwana Medvedev pia alionya kwamba hatua mpya zinazolenga kumuondoa rais Trump madarakani zitachukuliwa kwa kuwa sio mtu aliye na utaratibu.
Moscow ambayo imekana kuingilia uchaguzi wa Marekani tayari imelipiza kisasi wiki iliopita wakati bunge la Congress lilipopitisha muswada uliowatimua maafisa 755 kutoka katika ubalozi wa Marekani nchini Urusi mbali na kuzuiwa kutumia jengo moja la Marekani pamopja na ghala moja nchini Moscow.
Mataifa kadhaa ya Ulaya ikiwemo Ujerumani yanahofia vikwazo hivyo vipya na rais wa tume ya Ulaya Jean Claude Juncker ameonya kwamba athari yake itaathiri maslahi ya kawi ya Ulaya.
NIJUZE HABARI KWA 0625 966 236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: