AU yaichukulia hatua ya jeshi la Zimbambwe kuchukua madaraka na kumzuilia Mugabe kuwa ni mapinduzi ya kijeshi

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM.
Mkuu wa AU Alpha Conde

Hatua ya jeshi la Zimbabwe ya kuchukua madaraka na kumzuilia Rais Robert Mugabe, inaonekana kama mapinduzi ya kijeshi, Muungano wa Afrika AU umesema.
Mkuu wake, Alpha Conde, alisema kuwa AU inataka kurejea mara moja hali ya kawaida.
Jeshi linakana kufanya mapinduzi ya kijeshi, na kusema kuwa Mugabe yuko salama, na kuwa hatua zao ni dhidi ya waalifu wanaomzunguka.
Hatua ya jeshi inafuatia mvutano kuhusu ni nani atamrithi Bw. Mugabe.
Makamu wa rais, Emmerson Mnangagwa alifutwa kazi wiki iliyopita, na kuchangia mke wa rais Grace kuwa na fursa ya kumrithi Mugabe, hali iliyosababisha maafisa wa vyeo vya juu jeshini kuhisi kutengwa.
Bwana Mugabe 93, ametawala siasa za nchi tangu ipate uhuru kutoka Uingereza mwaka 1980.
Akijibu yale yaliyotokea Bw. Conde ambaye pia ni rais wa Guinea, alisema kuwa wanajeshi wa Zimbabwe walikuwa wamejaribu kuchukua madaraka.
Misri ilifukuzwa kutoka AU wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2013, kwa hivyo jeshi la Zimbabwe linaweza kuwa linajaribu kuzuia hali kama hiyo kw kutaja hatua yao kuwa isiyo mapinduzi ya kijeshi.
Tuma habari picha WhatsApp kwa 0625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: