Lowassa akana madai ya yeye kupiga hodi CCM

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>


Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Lowassa amesema amepata taarifa za uvumi unaosambazwa kuwa kuna watu amewatuma kuomba arudi CCM jambo ambalo ni uongo.

“Huu ni uongo wa kutunga, wamekuwa wakitunga vitu vingi juu yangu, mimi sina mpango wa kurejea CCM,” alisema Lowassa,ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
Amesema uongo mwingine ambao unasambazwa ni kuwa Serikali imezuia watu kumtembelea nyumbani kwake jambo ambalo anaamini ni maneno yanayotungwa.
“Watu wanazuiwa kuja nyumbani kwangu, eti Serikali imezuia hivyo wanakuwa wanaogopa huu ni uongo Serikali haiwezi kuzuia watu kutembeleana,” alisema
•Tuma habari picha WhatsApp kwa 0625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: